Rapa maarufu Cardi B ametangaza rasmi kuwa anatarajia mtoto wake wa nne, ikiwa ni wa kwanza na mpenzi wake, nyota wa NFL Stefon Diggs.
Akizungumza kwenye mahojiano na CBS Mornings yaliyorushwa Septemba 17, 2025, Cardi B, amesema ujauzito wake unakuja kabla ya kuanza kwa tamasha lake linalotarajiwa kufanyika Februari mwakani.
“Ninatarajia mtoto na mpenzi wangu Stefon Diggs,” alisema kwa furaha huku akimshukuru mtangazaji Gayle King kwa pongezi. “Nimejaa furaha, najisikia niko sehemu nzuri sana, nina nguvu na nina amani.”
Cardi B, tayari ana watoto watatu na rapa Offset: binti Kulture Kiari (7), mtoto wa kiume Wave Set (4) na binti mdogo Blossom Belle (1). Offset naye ana watoto wengine watatu kutoka kwenye uhusiano wake wa nyuma.
Kwa upande wake, Stefon Diggs, ambaye kwa sasa ni mchezaji wa timu ya New England Patriots, ana mtoto mmoja binti aitwaye Nova mwenye miaka 8.
Wawili hao walianza kuhusishwa kimapenzi tangu Oktoba 2024 na walithibitisha uhusiano wao Mei 2025 walipoonekana pamoja kwenye mchezo wa NBA katika Madison Square Garden.
Tags new trendingSubscribe Our Newsletter
0 Comment
Post a Comment
Your thoughts and opinions matter. Leave a comment below DO NOT SPAM!